Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti, amewataka wananchi kupuuza taarifa potofu

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Alexander Mnyeti, amewataka wananchi kupuuza taarifa potofu zinazodai kuwa samaki wanaofugwa kwa teknolojia ya vizimba hawana ubora ikilinganishwa na samaki wanaopatikana kupitia uvuvi wa asili, akisisitiza kuwa samaki hao wana ubora unaotokana na udhibiti wa aina ya chakula wanacholishwa.


Mnyeti ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuwawezesha mitaji vijana 85 wanufaika wa programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT-Uvuvi), wanaotarajiwa kujishughulisha na ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba mkoani Geita.

Amesema dhamira ya Serikali ya kuwekeza katika ufugaji wa samaki kwa teknolojia ya vizimba imesaidia kukabiliana na changamoto ya upungufu wa samaki nchini, huku ikifungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi, Merisia Mparazo, amesema programu ya BBT-Uvuvi ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya kuwawezesha vijana kupata ujuzi, mitaji na fursa za ajira kupitia shughuli za uzalishaji katika sekta ya uvuvi, ikiwemo ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.





Post a Comment

Previous Post Next Post