Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amewahimiza waandishi wa habari na Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT) kuwafikia wananchi waishio maeneo ya vijijini na kuandika shughuli zao.


Akifungua Kongamano la Mwaka na Tathmini ya Huduma za Habari na Mawasiliano Vijijini, lililofanyika Oktoba 31, 2026, mkoani Dodoma, Msigwa amesema waandishi wa habari ni sauti ya wananchi, hivyo wana wajibu wa kufikisha changamoto, mahitaji na mafanikio yao kwa jamii.

Amesema waandishi wana nguvu kubwa ya kuleta mabadiliko na kusisitiza kuwa kalamu zao zinapaswa kutumika kulinda maslahi ya taifa na wananchi badala ya kutumikia ajenda binafsi.

Katika mkutano huo wa mwaka wa RUJAT uliofanyika mjini Dodoma, Msigwa ameahidi kuchangia Sh milioni 10 kwa ajili ya kutunisha mfuko wa chama hicho.

Post a Comment

Previous Post Next Post