Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dkt. Batilda Burian, amesema kuna umuhimu wa kubadili mfumo wa biashara ya machungwa kwa kupiga marufuku ununuzi wa zao hilo moja kwa moja mashambani ili kuwalinda wakulima dhidi ya unyonyaji wa madalali.
Akizungumza katika kikao cha kutathmini namna ya kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la machungwa mkoani Tanga, amesema utaratibu bora wa biashara utawawezesha wakulima kupanga bei na kupata masoko yenye tija.
Amesema Tanga ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa machungwa nchini, hivyo ni muhimu kuhakikisha wakulima wanapata faida inayostahili kutokana na mazao yao.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA), Famia Hamisi, amesema mamlaka hiyo itaendelea kuboresha mazingira ya uzalishaji na biashara ya machungwa ili kuongeza manufaa ya kiuchumi kwa wakulima.
Post a Comment