Serikali imesema inatenga asilimia 10 ya mapato yote yatokanayo na sekta ya madini kwa ajili ya kufanya utafiti

 Serikali imesema inatenga asilimia 10 ya mapato yote yatokanayo na sekta ya madini kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina utakaosaidia kubaini maeneo mapya yenye rasilimali za madini nchini, kuongeza uhakika wa upatikanaji wa malighafi na kuvutia uwekezaji katika uanzishwaji wa viwanda.


Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema hatua hiyo inalenga kuongeza fursa za ugunduzi wa maeneo mapya yenye madini pamoja na kuwawezesha wachimbaji wadogo kuachana na uchimbaji wa kubahatisha na badala yake kutumia taarifa sahihi za utafiti ili kuongeza uzalishaji.

Amesema upatikanaji wa taarifa sahihi za rasilimali za madini utasaidia kuhakikisha viwanda vitakavyoanzishwa nchini vinakuwa na uhakika wa kupata malighafi za kutosha kwa ajili ya uzalishaji.

Aidha, Mavunde amesema hivi karibuni ndege maalumu za utafiti wa madini zitafanya kazi katika anga la Tanzania kwa lengo la kufanya utafiti katika maeneo mbalimbali ya nchi, yakiwemo Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya, Songwe, Lindi na Mtwara.

Amesema kupitia tafiti hizo, Serikali inalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya madini na kuwahamasisha kuitazama sekta hiyo kama moja ya nguzo muhimu za uchumi na maendeleo yao.


Post a Comment

Previous Post Next Post